Leo
nimeona ni vyema nika-share nanyi kisa hiki cha kutekwa mfanyakazi
mwenzetu ambaye ni cashier siku ya jumatano jioni wiki iliyopita.
Ni kama movie lakini ni ukweli, cashier wetu aliomba ruhusa siku hiyo ya
tukio aende kwenye mkutano wa wasabato uliokuwa uliendelea viwanja vya
biafra. Yeye pia ni msabato aliyeishika dini ya Sabato haswa, kwa hiyo
aliondoka saa kumi kamili badala ya saa kumi
na moja
Baada ya dakika 40 tulianza kupokea sms zinazosema mwenye namba xxx
amepata ajali na kufa papo hapo na kwa taarifa zaidi twende muhimbili
hospital. Baada ya kutazama hiyo namba xxx ilikuwa ni ya cashier wetu.
Tulijaribu kuipiga iliita tu bila kupokelewa, na
pia tulipiga namba iliyotutumia sms iliita bila majibu. Ilipofika saa
kumi na moja tuliamua kuelekea muhimbili, ma baada ya kufika pale
emergence tukaambiwa tuelekee chumba cha kuhifadhia maiti. Tulioneshwa
mwili wa mtu aliyepata ajali lakini haukuwa wa cashier
wetu, tukawatuma wenzetu waende hospitali zote lakini hapakuwa na
taarifa zake
Baada ya kuzunguka bila mafanikio tulitoa taarifa makao makuu ya usalama
barabarani na baada ya dk kumi wakatwambia kuwa hakuna taarifa za ajali
mbaya iliyotokea jioni hiyo. Hatua iliyofuata ilikuwa ni kutoa taarifa
polisi juu ya tulio hilo na ndipo waliposema
kwa kuwa ni mtu mzima tusubiri hadi siku inayofuata. Wakati huo huo
ndugu zake pamoja na wafanyakazi wenzetu walikuwa pamoja wakiendelea na
jitihada za kumtafuta hadi saa sita usiku. Kilichokuwa kinatia wasiwasi
zaidi ile namba iliendelea kutumia sms namba
takribani zote zilizokuwa kwenye phonebook yake na ndugu zake
hawakuwahi kuona ndugu yao akichelewa kiasi hicho.
Ilipotimu mida kama ya saa sita na nusu walisikia mtu akigonga mlango,
alikuwa kaumizwa na amejaa matope, hakuwa na uwezo wa kuzungumza sana,
ilibidi wampeleke kituo cha polisi na baada ya muda hospitali ya
mwananyamala.
Alipopata nguvu alianza kuwasimulia nduguze kilichotokea. Alipotoka
ofisini alikwenda moja kwa moja kwenye kituo cha daladala cha karakana,
pale kituoni walikuwa abiria wawili yaani yeye na mama mmoja. Baada ya
dk chache ilikuja coaster iliyoandikwa mbele Kawe
na ilikuwa na tinted nyeusi, yule mama hakupanda sababu alikuwa
anaelekea posta ila yeye alipanda. Ndani ya gari kulikuwa na watu watatu
pamoja na dereva, wawili wakiwa wamekaa nyuma na mmoja akiwa amekaa
karibu na driver. Gari hiyo hiyo ilikuwa ni mpya, mmoja
wa abiria alimumba simu cashier apige simu moja kwa jamaa yake maana
alidai kuwa simu yake illiishiwa charge na walikuwa wametoka mtwara
kupeleka maiti, alimuuliza cashier umri wake na kama ameoa na anafanya
kazi wapi, cashier akamjibu hajaoa na hana kazi
pia ana miaka 32. Walipofika Tazara hawakutaka kupakia abiria yoyote na
walikuwa wote wamevaa miwani myeusi, na ndipo akaanza kuingiwa na
mashaka akaomba ashuke, wao wakamwambia watapita
biafra na hawana mpango wa kusanya kwa kuwa hata yeye walimpa lifti tu.
Gari ilipokaribia taa za buguruni akainuka ili ashuke, jamaa wale wa
nyuma wakamkalisha chini kwa nguvu, na sio kwenye viti yaani chini
kabisa. Mmoja wao akafunga kitambaa cheusi kwenye
macho na mikono ikafungwa kwa nyuma na mipira, baada ya muda akasikia
kama wamempulizia perfume. Akihisi fahamu kumtoka polepole na neno
lamwisho analokumbuka alisikia kuwa waelekee misitu ya Kibaha wakamalize
kazi. Kilichomwamsha ni kofi zito alilopigwa na
kusukumwa hadi nje ya gari. Alianza kulia na kuwasihi wasimdhuru,
wakaanza kumrusha kichurachura huku wakimkanyaga. Walikuwa
wameshamfungua kitambaa machoni na waliacha gari umbali kama wa dk kumi
na lilikuwa ni pori zito na giza, wao walivaa vitu usoni na
walikuwa wamevaa gloves. Wakamwekea simu yake mfukoni wakiwa wametoa
simcard, walichomwambia wanachohitaji ni sehemu zake za siri na sio kitu
kingine. Mmoja wao akaambiwa alete kisu kikali
wanachokitumia, na walipompigia boss wao akawasisitiza nyeti
zinazotakiwa lazma ziwe za mtu wa miaka 40 na kuendelea. Mwenzao mmoja
akasema cashier alisema alikuwa na miaka 32, baada ya kumkagua wakakuta
card yake inaonyesha kazaliwa mwaka 1979. Kulingana na
yeye asemavyo ndicho kilichomwokoa ila waliendelea kumkung'uta kwa
hasira. Wakamrudisha kwenye gari na baada ya mwendo wakampakia kwenye
gari nyingine ndogo iliyokuwa na watu wawili ambao walimchukua na
kumtelekeza maeneo ya sayansi. Hawakuchukua kitu hata
kimoja wala kumwambia lolote,siku iliyofuata alipelekwa agakhan kwa
uchunguzi zaidi na kwa sasa anaendelea vzr.
Kwa ufupi ni hayo, ukweli mwenyezi Mungu atulinde na tumwombe pia
abadilishe mioyo ya watu ambayo imekuwa migumu mno kwa ajili ya kupata
vyeo na utajiri wa haraka
No comments:
Post a Comment