SHOSTI namba moja wa msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu, Snura Mushi
ameeleza kuwa, tangu amekuwa karibu na staa huyo amejikusanyia maadui
wengi bila kujua sababu.
Snura aliyasema hayo hivi karibuni
kwenye televisheni moja jijini Dar wakati alipokuwa akizungumzia ishu ya
kwamba yeye amegeuka kuwa bodigadi na mbeba mabegi wa Wema.
Alisema,
yeye na Wema ni marafiki walioshibana na wamekuwa wakisaidiana katika
mambo mengi lakini anashangaa kuona anachukiwa na watu.
“Inaniuma
sana, eti watu wanasema mimi ni mbeba mabegi na simu za Wema, wengine
wanasema mimi ni bodigadi wake. Mbaya zaidi wanafikia hatua ya
kunizushia mabaya na kunichukia bila sababu
Story Na Imelda Mtema-Global Publisher
No comments:
Post a Comment