Baada ya kuhisi kuwa mchina Ye Shiwen (16) atakua
ametumia madawa ya kuongeza nguvu apimwa na kuonekana safi.
Mwenyekiti wa Chama cha
michezo ya Olimpiki ya Uingereza amesema, baada ya shaka
la kocha wa Marekani (John Leonard
) kutolewa kuhusiana na kuwa mtu wa kawaida hawezi kuogelea kwa kasi
aliyoonesha Ye Shiwen na kuvunja rekodi ya dunia waliamua
kumpima na majibu kuonekana hakuwa na matumizi yoyote ya kutumia dawa za
kuongeza nguvu hivyo anastaili kutambulika ulimwenguni kwa rekodi hiyo.
Kocha
huyo wa Marekani alisema kitendo
cha kuogelea kwa kasi hiyo kulimchanganya na kuisi kuwa kuna swala hilo la
kutumia madawa. Kwani kitendo cha Ye
Shiwen,kilimkumbusha waogeleaji wa
Ujerumani Mashariki wanawake katika
miaka ya 1980, ambao walitumia madawa.
Ye Shiwen amevunja rekodi ya dunia kwa kuogela ndani ya sekunde 28:93 umbali wa m50 na
kumpita mmarekani mwanaume ryan
lochte(27) kwa sekunde mbili zaidi ambaye alishikilia rekodi hiyo kwenye
mashindano ya olympics
No comments:
Post a Comment