Wednesday, July 25, 2012

JOHN MAHAMA DRAMANI, AMBAYE ALIKUWA MAKAMU WA RAIS WA GHANA MWAKA 2009, AAPISHWA KAMA RAIS WA GHANA MARA BAADA YA KIFO CHA RAIS JOHN ATTA MILLS

Raisi wa  sasa wa Ghana, John Dramani Mahama

Zoezi la kuapishwa.

Raisi John Atta mills enzi za uhai wake


John Dramani Mahama  usiku wa jana apishwa kuwa  Rais wa Jamhuri ya Ghana na Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Jeshi nchini Ghana,  ambapo anachukua nafasi ya marehemu Rais Evans Atta Mills, ambaye alifariki dunia katika Hospitali ya Jeshi mchana Jumanne 24, baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kama ilivyoainishwa katika  kifungu cha 60 (6) ya Katiba ya 1992 ya Ghana, Jaji Mkuu Georgina Theodora Wood  wa Ghana alisimamia zoezi zima la kiapo cha Makamu huyo wa zamani wa Raisi, ambapo katika zoezi hilo kulitanda hisia za Majonzi.

Mara baada ya kuapishwa Raisi Mahama Alisema: "Kwa mara ya kwanza katika historia ya Ghana, tumepoteza rais aliyepo madarakani ambaye alifanya kazi bila kuchoka kwa ajili ya watu wake".

Rais Mahama alisema kamwe hakufikiri kuwa  angeweza kuongoza  taifa  katika kipindi kigumu kama hiko na kuwasihi wa Ghana kudumusha umoja na utulivu wa Taifa ". Raisi Atta Mills amefariki akiwa na umri wa miaka 68. Mungu ampumzishe kwa Amani.

No comments: