Monday, July 30, 2012

WANASAYANSI NCHINI MAREKANI, WAONGEZA MATUMAINI YA KUPATIKANA KWA DAWA YA KUTIBU UKIMWI!!


Kuna habari njema kuwa wanasayansi nchini Marekani wamegundua dawa inayotibu   ugonjwa wa Ukimwi.

Kwa mujibu wa BBC watafiti nchini marekani wanasema wamepata njia ya kutibu virusi ivyo vya ugonjwa wa ukimwi kwa kutumia dawa inayokinga ugonjwa wa saratani. 

Ugonjwa wa ukimwi umekua mgumu  kutibika kutoka na virusi hivyo kukaa muda mrefu mwilini bila kutambulia. Katika kurasa zao za jarida la matibabu ya asili( Natural) wataalamu hao wamesema, wamepata njia ya kuvimulika virusi hivyo mwilini na kuwa kitendo cha kufanya hivyo wameweza kuviua virusi kwa kutumia dawa za  kuongeza nguvu mwilini. 

Tayari majaribio yamefanyika kwa wagonjwa nane na kufanikiwa  huku wakiongeza kuwa, bado kunaitajika utafiti zaidi wa kuezesha kuundwa kwa dawa madhubuti ya kumaliza ugonjwa huo. Haya yote yametokea wakati watu wengi sasa wamekubali kua ukimwi upo na unaua.

No comments: