
BAADA
ya kutamba kwa muda mrefu katika muziki wa kizazi kipya nchini, msanii
nyota wa muziki huo, Naseeb Abdul ‘Diamond’ amesema anafikiria kujitosa
katika muziki wa taarab.
Diamond alisema Jijini Dar es Salaam wiki hii kuwa,amefikia uamuzi
huo kutokana na kuvutiwa na muziki huo wa taarab. Mshindi huyo wa tuzo
mbalimbali za muziki za Kilimanjaro amesema, anajua uamuzi wake huo
utawashangaza mashabiki wengi, lakini ni jambo la kawaida kwa msanii.
Diamond alisema hadi sasa anaamini hana mpinzani katika muziki wa
kizazi kipya na hakuna msanii anayeweza kufikia kiwango chake hapa
nchini. Diamond alisema ameamua kupiga miondoko tofauti ya muziki
kutokana na kipaji alichonacho katika fani hiyo, ambayo imempatia
umaarufu mkubwa, Kutokana na kipaji chake hicho,Diamond alisema hakuna
kitu anachoshindwa kukifanya katika fani ya muziki.
"Nashukuru mungu kwa kipaji, nahisi naweza kufanya aina yoyote ya
muziki, nitajaribu kwa kuwa nia yangu ni kufanya zaidi aya kile
nilichofanya sasa" alisema
Alisema bado hajaanza rasmi kupiga muziki wa taarab,na kuwa sasa
anafanya tathmini ya soko la muziki huo ili kuona kama unaweza kumletea
mafanikio kama ilivyo kwa muziki wa bongo fleva.
Alisema anaweza kufanya kila aina ya muziki kwa sababu anakipaji cha
kuimba nyimbo aina zote, hivyo endapo atafikia muafaka anaweza kufanya
muziki wa taarabu. Diamond alikiri kuwa, muziki wa kizazi kipya
umemfanya ajulikane sehemu nyingi duniani, ikiwa ni pamoja na kupata
manufaa mbalimbali kimaisha kwa kuishi kwenye nyumba nzuri na kumiliki
magari ya kifahari.
(kwa mujibu wa bongoflavalink.)
No comments:
Post a Comment