Friday, September 7, 2012

'HAUTAWEZA TENA KUMBUSU MWANAUME' - AUKATA MDOMO WA MKEWE


Mmoja wa madaktari anayeheshimika nchini Sweden ameukata mdomo wa mkewe aliyekuwa akililia talaka ili mkewe huyo asiweze tena kumbusu mwanaume yeyote katika maisha yake yote yaliyobaki. Daktari huyo bingwa mwenye umri wa miaka 52 aliwaambia polisi kuwa alichukua uamuzi wa kuukata mdomo wa mke wake mwenye umri wa miaka 32 kwakuwa mke wake huyo alikuwa aking'ang'ania kudai talaka.

Daktari huyo alichukua uamuzi huo baada ya mkewe kurudi nyumbani kutoka kwenye tripu ambayo inahisiwa alienda na mpenzi wake wa nje ya ndoa.

"Sikutaka kumuua, nilitaka ataabike maisha yake yote kwa haya aliyonifanyia", alisema daktari huyo bingwa anayeheshimika sana katika tafiti za kitabibu katika taasisi ya Karloinska Institute ya jijini Stockholm.

"Awali nilichukua kisu lakini hakikuwa na makali ya kutosha ndipo nilipochukua kisu chenye ncha kali kinachotumika kwenye upasuaji mahospitalini".

Daktari huyo aliongeza kuwa mkewe alikuwa macho wakati wa shambulio hilo na alimwambia kuwa anataka kumuadhibu sio kumuua.

"Niliuvuta mdomo wake na kuukata kwa kisu na kisha niliutafuna tafuna", alisema daktari huyo katika mahojiano na polisi.

"Awali nilifikiria kuwa kwa kuukata tu mdomo wake, madaktari wanaweza wakauunganisha tena ndipo nilipoamua kuutafuna na kuumeza ili kuzuia kutokea kwa hali hiyo", aliongeza dakatari huyo.

Magazeti ya Sweden yalisema kuwa daktari huyo aliwaambia polisi kuwa uamuzi huo aliuchukua ghafla na kuamua kuondoa udhia.

"Mimi ni mwanasayansi na nina IQ kubwa sana, nina uwezo wa kutatua matatizo ndani ya sekunde chache", alijigamba daktari huyo ambaye jina lake liliwekwa kapuni.

Awali polisi walitaka kumfungulia mashtaka ya kujaribu kuua kwakuwa shambulio hilo lilikuwa baya sana lakini mahakama ilipunguza ukali wa mashtaka hayo na kuwa mashtaka ya kufanya shambulio la kudhuru mwili.

No comments: