Monday, July 16, 2012

JE ULIKUWA UNAJUA KUWA MAMA WA MWANASOKA NYOTA BALOTELLI AMBAYE ANALIPWA£120,000 KWA WIKI NI MFANYAKAZI WA USAFI??

Huyu ndio mama yake Mario Balotelli




Wakati Mchezaji Nyota Balottelli akiingiza kiasi cha £ 120,000 kwa wiki, mama mzazi wa mchezaji huyo anafanya kazi kama mfagizi katika kampuni moja ya kukodisha Magari huko nchini uingereza na kuingiza £ 6 kwa saa. 


Mbali na kutoa sadaka nyingi kanisani kunywa vinywaji vya gharama  na kujiachia sana mwanakabumbu huyo haonyeshi ukarimu huo kwa mama aliyemzaa.


Balotteli ambaya ana asili ya  Ghana alikua adopted wakati akiwa na umri wa  miaka miwili huko nchini italia kutokana na ugumu wa maisha waliokua nao  wazazi wake.


Krismasi ya mwaka jana mama huyo mwenye umri wa miaka 46,  akiwa na binti yake ajulikanae kwa jina la Rose waliamia mjini Manchester kwa kile alichodai kuwa karibu na mwanae na si kwa kutaka kutumia utajiri wa mwanae au kingine chochote kwani anafurahia hali  yake ya maisha anayoishi.Mbali na hayo yote Mchezaji huyo amekua akionekana mara kwa mara akienda kumsalimia mama huyo.


1 comment:

Anonymous said...

hili ni fundisho kwa wamama wote ambao wanajifanya oh sijui ugumu wa maisha itabidi mtt akalelewe somewere ,wamama tulee watoto wetu no matter how situation kwa sababu kuna mother love ambayo mtoto akikosa inamsononesha maisha yake yote.