MTANGAZAJI
na mwigizaji maarufu Bongo, Ben Kinyaiya amekwaa skendo ya kumtapeli
Zeght Dibega ambaye alikuwa mpangaji mwenzake, Mwananyamala jijini, Dar.
Akizungumza na Motomoto Newz, Zeght alidai kuwa, mwishoni mwa
Julai, mwaka huu, alimpa Ben shilingi elfu 20 kwa ajili ya kununulia
umeme na wakakubaliana endapo atahamishwa kwa kuwa muda wake ulikaribia
kuisha, basi Ben atachukua fedha hiyo kutoka kwa mpangaji mpya na
kumrejeshea yeye lakini hata alipohama, staa huyo hakufanya hivyo.
Alipotafutwa Ben na kuulizwa kuhusu madai hayo alisema hivi:
“Huyo
dada ni mwongo mkubwa, alishagombana na wapangaji karibu wote, mimi
niliteuliwa kuchangisha fedha ya umeme, nikafanya hivyo na umeme
akautumia lakini nashangaa anadai nimemtapeli.
“Yeye pale alifukuzwa kwa sababu alikuwa haelewani na mwenye nyumba hadi wapangaji wenzake,” alisema Ben.
story na Global publishers!!
No comments:
Post a Comment