RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho
Kikwete amemuita ikulu mwanamuziki anayefanya vizuri kwa sasa kwenye Bongo
Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ na kumpa jukumu maalum, Ijumaa
linairusha hewani. Kwa mujibu wa Diamond, juzikati ‘prezidenti’ alimwita ikulu
Magogoni, Dar es Salaam na kumpa shavu la kwenda kufanya shoo kwenye mkutano
maalum utakaofanyika Washington DC nchini Marekani hivi karibuni. “Yaa, rais
aliniita akaniambia kuna shoo natakiwa kwenda kufanya Marekani. “Kwa mara ya
kwanza nitasafiri nje ya nchi na madensa wangu wanne na msemaji mmoja. Sasa
hivi hawataki kutembea na kupanda magari wasije wakakosa hiyo safari,” alisema
Diamond na kuongeza kuwa baada ya kuumwa, mawazo aliyaweka kwenye mchongo huo
hivyo mambo mengine yataendelea ikiwa ni pamoja na kufanya kolabo na
mwanamuziki wa kimataifa wa Nigeria, J. Martins.
No comments:
Post a Comment