KWA miaka mingi sasa, baadhi ya watu wamegubikwa na dhana potofu ya kwamba, kuwa mweupe ndiyo urembo .
Dhana hii imewafanya wengi waanze kutumia vipodozi vikali, bila kujali madhara ya baadaye.

Kwa mfano, hata baadhi ya wasanii, wake kwa waume, wamekuwa wakijibadili ngozi zao na tumewaona wakibadilika hatua kwa hatua.
Hata
hivyo, unapohisi kuna uzuri, mara nyingi kuna kudhurika. Madhara ya
awali ya vipodozi hivi, huonekana kwa mtumiaji kubabuka ngozi, kuwa na
mabaka meusi au ngozi kuwa nyekundu. Lakini yapo madhara mengine mabaya
zaidi ya hayo.
Kemikali hatari
Katika bidhaa hizo zinazotumika za kujichubua, kuna kemikali za aina mbili.
Kwanza ni ‘Hydroquinone’ na ya pili ni ‘Mercury’.

Hydroquinone kemikali hii ni sumu kali, ambayo hutumika kwa ajili ya kuchapisha picha na kutengeneza bidhaa za mpira.
Hutumika
pia kama kisaidizi katika kutengeneza rangi za nywele.Mercury nayo ni
kemikali ya sumu inayoweza kuuzwa katika maduka ya dawa pekee na kwa
kuidhinishwa na daktari.
Bidhaa hizi kwa muda mfupi huweza kuibadilisha ngozi yako kuwa nyeupe kwa kupenyeza na kuzalisha madini ya ‘melanin’

Madini
haya kiasili ndiyo humfanya mtu awe mweupe au mweusi. Katika matumizi
ya vipodozi vyenye kemikali hizo, awali mtumiaji huhisi kwamba tamanio
lake limekidhiwa, lakini ni lazima tuyaangalie kwa mapana madhara yake
ya baadaye.
Madhara
Kuzeeka mapema
Kadri mtumiaji atakavyoendelea kutumia vipodozi hivyo, atazalisha rangi hiyo kwa muda mrefu katika ngozi na ataanza kupata mabaka, au kuwa mwekundu.

Lakini pia, ngozi yake itazeeka kabla ya wakati.
Saratani
Kwa kuwa ngozi hulazimishwa kubadili rangi yake ya asili na ‘melanin’ kulazimishwa kuzalisha seli nyeupe ni rahisi kwa mtumiaji kupata saratani ya ngozi baada ya kipindi fulani.
Maradhi ya ini au figo
Madini ya ‘Mercury’, taratibu hujikita katika ngozi, kuingia katika seli zake na kubadili mwelekeo halisi wa kutengeza rangi ya ngozi.

Baada ya muda, madini hayo huaharibu ogani muhimu na kusababisha ini au figo la mtumiaji kufeli hata kusababisha kifo.
Ngozi kavu
Madhara mengine ya vipodozi hivyo ni ngozi kuwa kavu na wengine hutokwa na michirizi isiyopendeza mwilini.
Hata hivyo, wapo baadhi ya watu waliojikuta wakitumia vipodozi hivyo kwa lengo la kuondoa chunusi, mba, au maradhi mengine ya ngozi na badala yake wamejikuta wakibadilika rangi ya ngozi zao.
Watumiaji wa aina hii, wanatakiwa kusoma aina ya kipodozi kwanza, au kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa ngozi kwanza kabla ya kuchukua uamuzi wa kutumia vipodozi hivyo.
Wiki ijayo tutakuletea namna ya kuifanya ngozi yako iwe ang’avu kwa kutumia vipodozi asili vinavyopatikana nyumbani.

Shukrani Florence Majani wa Mwananchi.
No comments:
Post a Comment