
Kuna wengine wanaoa kwa sababu wameshinikizwa. Lakini ukweli ni kwamba ndoa yoyote ambayo haina upendo wa dhati, ni kosa kubwa.
Katika
hali kama hii baadhi ya watu huwa tayari kuoana na yeyote anayepita
mbele yake hata bila kuangalia kwa makini kama kweli mtu huyu ni mzuri
kwake au la.
Hali hii ya kukubali kuolewa kwa sababu wadogo zako
wameolewa, huchangia kasi ya ndoa kuvunjika, kwa sababu watu wanaoana
pasipo kupendana kwa dhati.
Ndoa ni nzuri, lakini lazima uelewe
kuwa unapaswa kuoana na mtu kwa sababu umemuona anakufaa hasa baada ya
kumchunguza kwa makini na kuamini kweli anakufaa.
Usiingie katika
mapenzi kwa unafiki, unafiki wa kusema aaah kwa vile baba amesema
nikikataa ataniona sina adabu....kumbuka ndoa ni maisha yako si ya baba
yako wala mama yako. Ukipata shida utakayeumia kimaisha ni wewe, si
mwingine.
Uongo pia ni suala baya katika uhusiano…mwingine ni
mnywaji mzuri wa bia na aina nyingine ya vileo lakini ukimuuliza
anakwambia mimi simwi wala sivuti, naye anakwambia aaah hata mimi bwana,
yaani sipendi kabisa kunywa.
Kama wewe ni mnywaji, sema mimi
nakunywa ili mwenzi wako ajue aina ya mke au mume ambaye atakuwa naye.
Ingawa ni hatari zaidi kwa mwanamke kulewa, kuliko mwanaume hasa katika
suala la uaminifu wa ndoa, lakini maisha ni makubaliano.
Ni rahisi
mwanaume mlevi kubaki mwaminifu, lakini ni vigumu kwa mwanamke mzuri
mlevi kubaki mwaminifu kwa ndoa yake, kama unabisha shauri yako.
Ninachotaka
kusisitiza hapa ni umuhimu wa mtu kuwa muwazi hasa pale wanapoanzisha
urafiki, hii itakusaidia hata katika siku za baadaye za uhusiano wenu
kuishi kwa amani.
Eeeh bwana maana mumeo atakuwa anajua kwamba
nimeoa mke mlevi, nimekubali, hakutakuwa na ugomvi, maana ulishamwambia
kwamba mimi bila kunywa usingizi haupandi...siku ukifungwa jela au
ukiumwa sijui utalalaje ? Mimi sijui, lakini ninachotaka kusema kwenye
kipengele hiki ni kwamba wapo watu wanasema hivyo kwamba eti asipokunywa
hajisikii vizuri, kitu ambacho si kweli.
Unafiki mwingine ni wa
tabia katika mazungumzo nk, ndugu yangu kama unaelekea kuoa au kuolewa,
ni vizuri siku moja tafuta uwezekano wa kugombana na mwenzi wako, uone
kauli zake zikoje, anajibu vipi malalamiko.
Kuna wengine
wanajifanya wakimya, lakini wana lugha chafu kana kwamba wametoka kwenye
shimo la choo. Ni wiki mbili tu zilizopita kuna mama mmoja alimchukua
binti kanisani awe mfanyakazi wake wa ndani.
Huyo binti alikwenda
kanisani, kweli walikuwa wakimsifia kuwa ni mzuri kwa namna alivyokuwa
akionekana....siku moja kwa bahati mbaya bosi wake alipata safari ghafla
kiasi kwamba aliacha fedha kidogo nyumbani.
Akiwa huko mbali na
nyumbani akapata ujumbe mfupi kutoka kwa mfanyakazi huyo wa ndani ??ndio
fedha gani hiyo umeniachia, mimi huwa sinywi maji ya bomba, nitumie
fedha ya kutosha ninunue maji ya dukani, nikinwa ya bomba tumbo linauma?
Huo
ni ujumbe wa kutoka kwa binti ambaye kanisani anaonekana ni mtakatifu.
Kama hiyo haitoshi wakati bosi wake yuko mbali ikabainika akawa analala
na kijana mmoja wa mtaani hapo, bosi akalazimika kumfukuza kwa sababu ya
kuona anakwenda kinyume na alivyokuwa akimtarajia.
Unafiki hauko
tu katika mapenzi, bali hata maofisini, mwingine anaweza kukuchekea na
ukaamini ni rafiki, kumbe anakuchimba...eeeh bwana wengine ni maarufu wa
kutangaza mabaya ya wenzao, huku wao wakijiona ni watu safi, wajuaji wa
mambo nk.
Katika maisha ni vizuri kuwa kama ulivyo, simamia
kwenye ukweli wala usikubali kuingia kwenye uongo ili upate hiki na
kile, maisha tunayoishi ni mafupi, uko leo, hujui kama kesho utafika,
yanini kuwa mnafiki? Yanini kusengenya wengine? Yanini kuwa mtu wa
majungu, badala ya kuangalia mambo yako ambayo yatakusaidia uwe na
maisha bora zaidi kuliko ulivyo sasa?
Tangu mwaka uanze umeshateta
watu wangapi? Umeshafanya unafiki mara ngapi? Je, kati ya maneno
unayozungumza kwa siku, mengi ni ya aina gani....unafiki, uongo au heri
kwa wengine? Mimi sijui, lakini wewe unalo jibu, lakini kwa vyovyote
itakavyokuwa ni vizuri katika maisha pendelea kuachana na tabia za
kinafiki.
Shukrani Mwananchi.
Shukrani Mwananchi.
No comments:
Post a Comment