MWANAMKE
anayedaiwa kusababisha ndoa ya Mtangazaji wa Redio ya Times FM ya
jijini Dar es Salaam, Khadija Shaibu ‘Dida’ na mumewe Gervas Mbwiga ‘G’
kuvunjika ametajwa kuwa ni Tecla Benedict, Amani limejazwa data za
kutosha.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mwanamke huyo ametajwa kuwa ni
chipukizi wa Bongo Fleva akiwa mwanafunzi wa chuo kimoja kilichopo
jijini Dar.
Kikitoa undani wa kisa cha ndoa hiyo kuvunjika, chanzo
chetu hicho kimesema kuwa, Tecla alituma ujumbe mfupi wa maneno (sms)
kwa mume wa mtangazaji huyo na kunaswa na Dida.
“Dida alianza
kuchati na Tecla bila ya mwanamke huyo kujua kama alikuwa akichati na
mwanamke mwenzake na kuweka bayana kwamba alikuwa mjamzito kitendo
kilichomchefua Dida,” kiliendelea kusema chanzo hicho.
Kikasema kuwa,
kesho yake Dida alimpigia simu Tecla na kumwagia matusi na kumpa
vitisho huku akimwambia kuwa ajiandae kuachiwa mume.
Baada ya kuona hivyo, Tecla alilazimika kubadili namba ya simu kwa kuhofia kuendelea kuandamwa na Dida.
Mwandishi
wetu baada ya kupata habari hizi, alimpigia simu Tecla ambaye alikubali
kuwa na uhusiano na mume wa Dida, G huku akidai kuwa hakuwa akifahamu
kama mwanaume huyo ni mume wa mtangazaji huyo.
“Siyo kosa langu
kwani hata siku moja sikuwahi kumuona na pete, nilipomhitaji wakati wote
alikuwa karibu na mimi, wala hakuwahi kuniambia kama ameoa,” alisema
Tecla.
Mwandishi wetu pia, alimvutia waya G na kumuuliza kama ni
kweli Tecla ndiye chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yake na Dida, hata
hivyo G hakutoa ushirikiano wa kutosha.
“Naomba unipigie baadaye kwani muda huu utanikosesha umakini, niko kwenye kikao, tutaongea baadaye,” alisema G na kukata simu.
Dida alipotafutwa alisema kuwa, hakuwa tayari kuzungumzia habari hizo kwa kuwa ameshaachana na mwanaume huyo.
“Tafadhali ndugu sina muda wa kuzungumza masuala hayo, niko serious (makini) na mambo yangu ya msingi…” alisema.
Ndoa ya Dida na G ilivunjika hivi karibuni baada ya kutimiza mwaka mmoja, awali ilidaiwa kuwa ilikuwa ni ndoa ya mkataba wa mwaka mmoja.
No comments:
Post a Comment