Wednesday, June 6, 2012

JE WAJUWA VIUNGO MBALIMBALI KATIKA CHAKULA VINAFAIDA KATIKA AFYA YA MIILI YETU. FUATANA NAMI UPATE KUJUA MATUMIZI YAKE NA FAIDA ZAKE!

Kitunguu saumu  (Garlic)    
 

Kitunguu saumu ni kiungo ambacho kimekuwa maarufu kwa matumizi
mbalimbali. Vipo vitunguu saumu vya rangi nyeupe ambavyo mara
nyingi huwa na tumba kubwa ambazo ni chache. Vingine ni vile vyenye
rangi ya zambarau au pinki ambavyo huwa na tumba ndogo
na nyingi. Vitunguu hivi vina ubora sawa.
Kitunguu saumu hufaa katika matatizo mengi
kama kusaidia kuzuia maambukizi yatokanayo
na bakteria, baadhi ya virusi na fangasi hasa
katika utumbo, mapafu na sehemu za ukeni.
Vilevile husaidia katika uyeyushwaji wa chakula,
kuzuia kuharisha na pia hupunguza fangasi za kinywani,
maambukizi katika koo na hata mkanda wa jeshi.


Kitunguu saumu kinaweza kutumika katika mapishi ya chakula, chai au
kinywaji chochote cha baridi au cha moto. Mtu anapotumia vitunguu
saumu atumie kwa kiasi. Inashauriwa kutumia vitumba visivyozidi sita
kwa siku hasa kama vitatumika vibichi

  

Tangawizi (Ginger)  

Tangawizi ni kiungo ambacho kinatokana na mizizi ya mmea wa
tangawizi. Kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au kikiwa
kimekaushwa na kutengenezwa unga. Tan g a w i z i inaweza kutumika katika vinywaji vilivyochemshwa.
Pia huweza kuongezwa kwenye vinywaji vingine au
kwenye chakula. 

Tangawizi husaidia kuongeza hamu ya kula,
kupunguza kichefuchefu, kutapika, kuharisha,
maumivu ya tumbo na gesi tumboni. Pia husaidia
uyeyushwaji wa chakula tumboni. Vilevile husaidia wakati wa
matatizo ya mafua au flu.


Iliki (Cardamom)
 

Iliki ni mbegu zinazotokana na mmea wa iliki ambazo
hutumika kama kiungo. Mbegu hizi huweza kusagwa
au kutwangwa na kuongezwa kwenye chakula au
katika vinywaji.
Iliki ni nzuri katika kusaidia kupunguza maumivu,
kichefuchefu au kutapika. Pia husaidia uyeyushwaji
wa chakula na huongeza hamu ya kula.


Mdalasini 

Ni kiungo kinachotokana na magome ya
mmea wa mdalasini. Kiungo hiki huweza kusagwa
au kutumika bila kusagwa. Vilevile mdalasini
h u weza kuongezwa kwe n ye chakula au katika
vinywaji vilivyochemshwa au baridi.


Mdalasini huweza kusaidia kupunguza matatizo kama mafua au flu,vidonda vya kinywani na hata fangasi za ngozi. Vilevile kiungo hiki huongeza hamu ya kula, pia husaidia kupunguza baadhi ya matatizo katika mfumo wa chakula kama kichefuchefu, kutapika au kuharisha.
 

Kinywaji kilichochemshwa chenye mchanganyiko wa mdalasini na tangawizi kinaweza kutuliza kikohozi.


Giligilani (Coriander)
 

Giligilani ni aina ya kiungo ambacho
majani na mbegu zake huwez a
kutumika kama kiungo katika mapishi
ya vyakula mbalimbali kama nyama,
supu au mchuzi. Kiungo hiki husaidia kuongeza hamu ya kula na kupunguza gesi tumboni. Pia husaidia kuzuia maambukizi ya bakteria na fangasi.
 


Kotimiri(Parsley)

Kotimiri ni aina ya mmea ambao majani yake na mbegu
zake huweza kutumika kama kiungo katika vyakula.
Majani ya kotimiri husaidia kupunguza msokoto wa
tumbo ambao mara nyingi hausababishi kuharisha.
 

Vilevile kiungo hiki huchochea vimeng’ e n yo
tumboni na hivyo kuongeza hali ya kuhisi njaa.
 

Mbegu za kotimiri huweza kusaidia kuondoa maji ya
ziada katika mwili. Kiungo hiki huweza kuongezwa
katika chakula wakati wa kupika au wakati wa kula.


Karafuu (Cloves)
 

Karafuu hutokana na mmea wa mkarafuu. Kiungo
hiki huweza kutumika peke yake au kwa
kuchanganya na viungo vingine. Kiungo hiki
husaidia kuleta hamu ya kula na kubores h a

uyeyushwaji wa chakula tumboni. Vilevile karafuu husaidia kupunguza
kichefuchefu, kutapika na kuharisha.
Ni nzuri ikitumiwa katika supu, mchuzi, juisi ya matunda yenye
uvuguvugu au vinywaji vingine vilivyochemshwa


Binzari (Turmeric/Yellow Root)
 

 Binzari halisi hutokana na mizizi ya mmea wa binzari
manjano ambao hufanana na ule wa tangawizi. Mizizi ya
binzari huweza kukaushwa, kusagwa na kutengeneza
unga wa binzari ya manjano ambao hutumika kama
kiungo cha chakula. Vilevile binzari mbichi
inaweza kutwangwa na kutumika kwenye
mapishi mbalimbali. Binzari ikitumiwa katika
chakula, hukifanya kuwa na rangi ya njano.
Binzari inaweza kutumika kwenye mapishi ya wali au
vyakula vingine vya nafaka, pia kwe n ye mchuzi au
maharagwe.
Binzari husaidia katika uyeyushwaji wa chakula na pia husaidia mwili
usiharibiwe na kemikali mbaya.
Ni vizuri kuwa waangalifu tunaponunua binzari ile ya unga kwani
wakati mwingine wauzaji huuza binzari ambayo si binzari halisi.
Binzari hii ambayo si halisi hutengenezwa kwa kutumia aina za
unga wa nafaka ambao huchanganywa na rangi ya manjano na
binzari kidogo.


Limau (Lemon)
 

Limau linaweza kutumika kama kiungo katika
chakula na vinywaji kama chai au vinywaji vingine.
Limau husaidia kuboresha uyeyushwaji hasa wa
protini na mafuta. Limau pia huweza kutuliza vidonda
vya kooni, kikohozi, homa na kuondoa msongo.



Binzari nyembamba (Cumin seeds)
 

Hizi ni mbegu nyembamba ambazo hufanana na mbegu za
giligilani. Mbegu hizi huweza kusagwa na kutengeneza unga
ambao hutumika kama kiungo katika mapishi mbalimbali
mfano; supu, mchuzi, wali, n.k.
Kiungo hiki husaidia kuongeza hamu ya kula, kupunguza
maumivu ya tumbo na hata kuharisha


 Mrehani (Basil)

Mrehani ni aina ya kiungo ambacho huweza kutumika kwa kuongezwa katika chakula. Kiungo hiki husaidia
kupunguza kichefuchefu na kusaidia uyeyushwaji wa chakula na kutuliza maumivu ya kichwa. Kwa vidonda vya kinywani mrehani unaweza kutumika
kwa kusukutua.


 Calendula
Vikonyo vya maua ya ‘‘calendula’’ vina kemikali inayozuia kukua kwa vijidudu kama bakteria katika jeraha, ngozi na pia kupunguza hali ya mwako wa moto (anti-inflammatory function). 

 Vilevile “c a l e n d u l a” hupunguza maambukizi
mbalimbali katika mfumo wa chakula.
‘‘ C a l e n d u l a’’ inaweza kutumika kutibu vidonda. Vilevile inaweza kutumiwa kama kinywaji kilichochemshwa ili kuboresha uyeyushwaji
wa chakula tumboni.



Pilipili (Cayenne)
 
“Cayenne” ni mchanganyiko wa aina za pilipili za jamii
ijulikanayo kama “capsicum”. Pilipili hizi huwa ndefu na
nyembamba, mara nyingi huwa ni kali na zina rangi
nyekundu. Jamii hii ya pilipili huweza kukaushwa na
kusagwa na hivyo kutengeneza unga laini ambao huwa
na rangi nyekundu.

“Cayenne” huweza kuongeza hamu ya kula. Pilipili hii inaweza ikatumika kwa kuongezwa kwenye chakula wakati wa kupika au wakati wa kula. Pia huweza kuongezwa katika juisi au maji ya kunywa. Hata hivyo ni vyema pilipili itumiwe kwa kiasi





Shamari (Fennel)
Shamari ni kiungo ambacho mbegu zake hufanana na zile za binzari
nyembamba. Kiungo hiki husaidia kuongeza hamu ya kula nakupunguza gesi tumboni.
Shamari inaweza kutumika kama kiungo kwenye
chakula. Mbegu za shamari zinawez a
kutumika kuandaa chai au kinywaji chochote
cha moto.Ni vizuri ikitumiwa kwa kiasi.


Nanaa (Mint)
 

Nanaa ni majani ya mnanaa ambayo hutumiwa kama kiungo.
Nanaa husaidia katika kuzuia hali ya mwako wa moto tumboni, kupunguza kichefuchefu, kuzuia kutapika na kuharisha. Pia huweza kupunguza maumivu ya tumbo na mkakamao wa misuli. Vilevile nanaa husaidia katika
uyeyushwaji wa chakula tumboni.
Nanaa iliyooshwa vizuri kwa maji safi na salama inawez a
kutafunwa. Vilevile inaweza kutumika kutengeneza kinywaji chamoto au kusukutua wakati mtu anapokuwa na vidonda kinywani


Meti (Methi)
 

Meti ni majani ya mmea uitwao kwa Kiingereza
“Fenugreek”. Hii ni aina ya kiungo ambacho huchochea uvunjaji wa kemikali mwilini yaani
umetaboli. Majani ya meti yanaweza kukaushwa na kutumika kama kiungo au kutumika yakiwa mabichi. Vilevile mbegu za “Fenugreek” huweza kukaushwa, kusagwa na kutumika katika kutengeneza unga wa viungo yaani “curry powders”. Meti inaweza kutumika kama kiungo katika vyakula mbalimbali ikiwa ni pamoja na mboga za majani na vilevile katika mapishi mbalimbali ya samaki.
 

“Thyme”
Inaweza kuzuia maambukizi yanayosababishwa na
bakteria au fangasi. Vilevile kiungo hiki husaidia kupunguza
kikohozi na kulainisha koo. Zaidi ya hayo “thyme” husaidia
ukuaji wa bakteria wazuri wanaosaidia katika uyeyushwaji wa chakula tumboni. Inaweza kutumika kama kinywaji cha moto au kusukutua





Shukrani kwao Center for Councelling, Nutrition and Health Care. wakati mwengine nitawaletea jinsi ya kutengeneza baadhi ya vinywaji vya viungo.

2 comments:

Unknown said...

Ahaa mimi sikujua hayo yote!

jackilawe said...

thanks mrs mlaki na kweli vingine hatuvijui twaviona masokoni tu kumbe vya tuhusu.