Siku chache baada ya msanii mwenye vibweka vingi ndani ya tasnia ya
filamu Bongo, Wema Abrahamu Sepetu kutangaza kuwa anamiliki mjengo wenye
thamani ya shilingi za kibongo Ml 400, hatimaye mmiliki halisi wa
mjengo huo ameibuka.
Akizungumza na Teentz.com mapema leo,mmoja watu walio karibu na
mmiliki huyo mwenye asili ya kiarabu anayemiliki jina la Ahmed au
Msafiri kama anavyojulikana kwenye mitaa hiyo amesema kuwa Wema
aliutangazia umma juu ya umiliki wake kwa nyumba hiyo wakati ambao
kijana huyo wa kiarabu alikuwa safari nchini Brazil kwenye michongo
yake.
“Unajua Wema amewadanya watu kwa kiasi kikubwa, nafikiri anatakiwa
kuomba radhi nakuwaeleza ukweli kwenye nyumba ile hana hata kipande cha
tofali na mmiliki halisi ni mshikaji wangu Ahmed ambaye mara kadhaa huwa
anasafiri kwenda nchini Brazil kibiashara” kilisema chanzo hicho.
Story na Teen News
No comments:
Post a Comment