Friday, August 3, 2012

MISS TANZANIA AISHIA ROBO FAINALI TOP MODEL



Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Miss World 2012, Lisa Jensen, ameishia hatua ya robo fainali ya shindano dogo la Top Model, ambalo limetoa vimwana 47 watakaochuana Agosti 12 ili kupata wanafainali 15 watakaoenda kuwania taji hilo siku ya fainali ya Miss World.

Fainali za 62 za Miss World zitafanyika Agosti 18 nchini China.

Washiriki 116 kutoka kote duniani watachuana kuwania kuwania taji hilo, na kufanya idadi kubwa zaidi ya warembo kupata kushindania taji hilo katika historia ya shindano hilo.


Miss World 2011, Ivian Sarcos wa Venezuela atamvisha taji mrithi wake katika shindano hilo.

Kwa mujibu wa tovuti rasmi ya Miss World, Lisa aliishia katika robo fainali pamoja na vimwana wengine tisa, Remona Moodley (Afrika Kusini), Laura Beyne wa Ubelgiji, Saly Aponte Tejada (Jamhuri ya Dominic), Delphine Wespiser (Ufaransa), Ines Putri Tjiptadi Chandra (Indonesia), Sonia-Lynn Gabriel (Lebanon), Daniela Darmanin (Malta), Sherlyn Ferneau (Shelisheli) na Claudine Book wa Marekani.

Ni washiriki sita tu kutoka Afrika walioingia katika nusu fainali hiyo yenye vimwana 47, ambao ni kutoka nchi za Kenya, Nigeria, Gabon, Sudan Kusini, Ivory Coast na Angola.
  
Michuano ya Miss World mwaka huu inahusisha mataji madogo ya Mrembo wa Ufukweni, Michezo, Urembo kwa Malengo, 'Multimedia Award', Tuzo ya Mbunifu wa Mitindo na 'Top Model'.

Shukrani Nipashe kwa story

No comments: