MSANII ‘first class’ wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Rehema Chalamila
‘Ray C’, amerejea Bongo na kutangaza kusaka mume huku akiweka wazi
vigezo anavyotaka awe navyo, Jelard Lucas anashuka nayo.
Akichonga na
Over The Weekend juzikati, Ray C aliyekuwa amejichimbia nchini Kenya,
alisema mwanaume atakayeweza kupata penzi lake anatakiwa kuwa na elimu
ya kawaida, maendeleo, asiwe mwanamuziki wala pedeshee, awe na mvuto na
mwenye kuyajua vizuri malavidavi.
Mwanadada huyo ‘chakaramu’
aliongeza kuwa mwenye sifa hizo akipatikana, atamzalia watoto wawili na
kujenga naye familia bora kwani amechoshwa na maisha ya usela.
“Sina
mume wala mpenzi, kwa sasa nipo single, ukiniulizia ishu za zamani
ntakushangaa kweli, vigezo ndiyo hivyo, kama kuna mtu yupo tayari
ajitokeze tufunge ndoa,” alisema Ray C.
Kuhusu kurudi kwenye gemu,
Ray C aliwaahidi mashabiki zake kuwa baada ya mfungo kumalizika, yupo
kwenye harakati za kuzindua albamu yake mpya aliyoipa jina la ‘Moyo
Waniuma’ yenye nyimbo 10.
Aliongeza kuwa soko la muziki Bongo ni bovu
sana ukilinganisha na Kenya hivyo bado mishemishe zake nyingi atakuwa
akizifanyia nchini humo
No comments:
Post a Comment