Watu wawili bibi na kijana wakiwa wamemeza madawa ya kulevya(Cocain) majina kapuni walizidiwa ghafla na kuanza kuomba msaada mara baada ya kufika sehemu ya kuondokea abiria kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere International Airport(JNIA).
Mkasa ulikuwa kama ifuatavyo mama mmoja anayekadiriwa kuwa na miaka 55 na kijana anayekadiriwa kuwa na miaka 33 walipokuwa wakichekiwa tiketi zao mama huyo alikuwa anahaha huku na huko akiwa anahitaji kukaa sehemu yenye baridi zaidi.
Mara baada ya kuangaliwa ticket zao walipanda sehemu ya kusubiria wageni ili waweze kuondoka lakini walipokuwa sehemu hiyo mama huyo alienda kununua cocacola na kuinywa na matatizo ndipo yalipoanzia hapo.
Mama huyo alianza kutokwa na povu la ajabu mdomoni. Hata hivyo watu wa usalama walijitahidi kumuuliza kuhusiana na madawa ya kulevya alikataa kata kata mpaka walipoanza kumbana kijana aliyekuwa naye ambaye alielezea kila kitu na kwamba mzigo wa madawa ya kulevya waulikuwa wakiupeleka Japan.
Kijana huyo aliongeza kuwa walimeza madawa hayo ya kulevya wiki moja iliyopita lakini walikosa ndege ya kusafiri hadi jana walipofanikiwa kupata ndege kwaajili ya safari yao ya Japan.
Watu wa usalama walijitahidi kuokoa maisha ya mama huyo ambaye hali yake ilizidi kuwa mbaya kadri muda ulivyosonga mbele na alifariki dunia kabla ya kufikishwa hospitali.
Kijana huyo naye aliwahishwa hospitali ila kwa maelezo ya daktari aliyemfanyia uchunguzi kupona kwa kijana huyo ni bahati maana vidonge vilikuwa vinaanza kutoka kupitia mdomoni.
Kijana huyo ana mke mwenye mimba ya miezi 8 na ana nyumba Sinza na Tegeta kwa kazi hii ya unga. Taarifa hizo zilijulikana kutokana na kauli za kijana huyo alizokuwa anatoa.
No comments:
Post a Comment