Nataka 2015 nikagombanie Ubunge
Kigoma , swali kugombania ubunge Kigoma ni Lazima niwe mzawa wa Kigoma? ilov
Kigoma,” ni tweet ya mtangazaji wa Clouds FM, Loveness aka Diva aliyoandika saa
sita mchana Jumapili hii.
Kama watu wengi walivyomzoea,
walijua ameamua kujifurahisha tu kwa kuandika kitu ambacho kamwe hakiwezi.
Lakini Diva alionesha kuwa huo sio
utani na kweli amedhamiria. ‘This is not a Joke , nataka kugombania ubunge
Kigoma 2015 , Diva future North Kigoma MP, anyone got a Qn, ask! Nantashinda,”
alisisitiza.
“Na ntatumia njia inaitwa strength
of a woman, u should put that woman first mind games tu and coz got mad lov for
kigoma#mpalltheway.”
Kwanini anataka kugombea Kigoma na
sio sehemu nyingine? “People wako nice, charming , wanaheshima, wanakubali cha
kwao na wana support,” alifafanua.
“Coz Kigoma kuna ardhi, mbuga za
wanyama, lake Tanganyika uvuvi and what more??? Vitu vingi sana ,ntasema.”
Amedai kuwa hivi sasa anajifunza
Kiha na hivi karibuni ataenda mkoani humo.
“Diva Kigoma future MP, my campaign
manager atakuwa@linex_tz , he is training me hicho kilugha cha Kigoma, soon
ntaenda.”
Katika
kile hackishness watu wengi kumpuuzia kwa kauli hiyo, walimuuliza
maswali ambayo mengi yalikuwa ya kejeli lakini alijibu kusisitiza nia yake na
kuanza kujinadi.
‘Najua ntaimarisha vipi elimu, ajira
na kilimo, nataka wajiajiri na biashara ndogondogo ,mikopo midogo midogo
itawasaidia sana.”
“Kwanini nishindwe? Labda nikuulize!
Nani kakwambia navaa high heels 247? Nani kakwambia siwezi zunguka vijijini?”
alimtupia swali mmoja aliyeonesha mashaka naye kwa kumchukulia kama sista duu!
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto
Kabwe wa jimbo ambalo Diva ataliwania kwa madai kuwa yeye atakuwa ‘rais
mtarajiwa’ ameonesha kumuunga mkono mtangazaji huyo kwa kusema, “Kila raia
mwenye sifa za kikatiba anaweza kuwa mbunge. Bunge linareflect jamii. Acha watu
wawe huru kusema watakacho. Hakuna ujinga ulio ujinga mtupu, hata ktk ujinga
kuna kujifunza.”
Naye Diva aliongezea, “Am free to
say whatever I believe kinafaa. As long As sijamtukana mtu, nasema nautaka
ubunge Kigoma by hooks and cooks. Ndo nshachagua huko sasa , no one can fight
me or change me, maamuzi, nakutaka sana huko kigoma ndo uamuzi wangu. Mimi sio
mzawa ni mzalendo, tunavunja imani ya uzawa ili tulete mabadiliko, ntajiunga na
chama kitanipitisha,wananchi watakubali.”
Mjadala uliendelea kuwa mzito. ‘Bado
nina mashaka sana kukumbusha tu wanawake wangapi waligombania majimbo
wakashinda mpaka sasa ndo tuendelee,” aliambiwa na mtu mmoja nay eye kujibu,
“Walishindwa wao, ungenijua ungejua nilivyokuwa na misimamo mikali na sitetereki,
nina jiamini, nguzo ya mwanamke kujiamini.”
“Last but not least ! No one can
fight me, by hooks and cooks, Diva for kigoma as future MP, vote vote vote ,
muda ukifika!”
Alimalizia kwa kusema, “It was only
a teaser, sneak peak #staytunned2015. #nishatangazania#overthisconvo.”
No comments:
Post a Comment