STAA wa filamu nchini, Wema Sepetu ameamua kufunguka kwa kusema kuwa
anakerwa na watu wanaotumia jina lake katika mitandao mbalimbali ya
kijamii ukiwemo wa Facebook, kwani wanamuharibia mambo yake mengi.
Wema ameliambia gazeti hili kuwa ana zaidi ya miezi 12 tangu alipojitoa
kwenye mtandao wa Facebook, lakini bado kuna mtu anatumia jina lake
vibaya kwa kuomba fedha kwa watu jambo ambalo linamkera kupita kiasi
kwani amekuwa akipigiwa simu na watu wakimuuliza kulikoni.
“Yaani
nakerwa sana na watu wanaotumia jina langu kutapeli au kuomba fedha
kwenye mtandao, halafu nawaomba wale waandishi wa blog wanaoandika stori
zao na kudai wamezungumza na mimi kumbe siyo kweli, waache upuuzi huo.
“Mashabiki wangu wakiona mtu anatumia jina langu kwenye Facebook wajue huyo ni tapeli na siyo mimi,” alisema Wema.
story na Global Publishers!!
No comments:
Post a Comment